 
Coastal union tayari kuwakabili wakatamiwa wa Mtibwa Sugar, mkwakwani Tanga.
Katika uwanja wa mkwakwani jijini Tanga wagosi wa kaya Coastal union watakua nyumbani kuwakabili wakata miwa wa Mtibwa Sugar. Na katika dimba la kaitaba Kagera sugar wanankurukumbi watakipiga dhidi ya wauaji wa kusini Namungo FC. Mechi zote hizi zitapigwa majira ya saa 10 kamili jioni.

wachezaji wa yanga wakiwa mazoezini kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Biashara united jumanne hii.
Michezo mingine ya hatua ya 16 bora Azam sports federation itaemdelea tena kesho kwa michezo miwili majira ya saa 10 jioni Tanzania prisons watakua nyumbani kuwakaribisha maafande wenzao wa Polisi Tanzania, ma mchezo mwingine utapigwa majira ya saa moja usiku ambapo timu ya wananchi klabu ya Yanga itakua nyumbani kuwakabili Biashara United toka mara.

 
 

 
 
 
 
 
